SASA POP 8 IPO MADUKANI
Habari njemani kwamba TECNO imetangaza rasmi uzinduzi wa simu mpya kwenye mfululizo wa Pop, TECNO Pop 8. Sasa inapatikana katika maduka yote nchini kwa bei nafuu. Simu hii ina huduma za ubunifu na muundo wa kuvutia, ikiahidi kuleta mabadiliko katika uzoefu wa matumizi ya simu kwa watumiaji duniani kote. Toleo jipya la POP 8 linajitokeza kama mojawapo ya simu bora yenye sifa nzuri. Muundo wake mwembamba na wa kisasa, pamoja na betri inayodumu kwa muda mrefu, hutoa ufanisi wakati wa shughuli za kila siku. Kipengele cha pekee cha DUAL SPEAKER kinaboresha ubora wa sauti kwa kutumia mfumo wa speaker mbili kwenye POP 8, na pia ina uwezo wa DYNAMIC PORT. Sasa, TECNO Pop 8 inapatikana kwa urahisi katika maduka yote nchini. Hii ni hatua kubwa katika ulimwengu wa simu za mkononi, ikileta muundo mwembamba, utendaji wa nguvu, na bei nafuu kwa watumiaji.